Viongozi wawili wa dini nchini Canada wamepatikana na hatia ya kuoa wake wengi.
Mahakama iliambiwa kuwa Winston Blackmore mwenye umri wa miak 61 alioa wanawake 24 naye mwanamume ambaye alikuwa ni mkwe wake James Oler akaoa wanawake 5.
Wote walipatikana na hatia ya shtaka moja la kuwaoa wanawake wengi na kila mmoja anakabiliawa na kifungo cha miaka mitano jela.
Hukumu hiyo imetajwa kuwa mtihani mkubwa kwa uhuru wa kdini nchini Canada.
Blackmore na Oler ni kutokna jamii moja ya dini ya karibu watu 1500 ambayo ilianzishwa mwaka 1946.
Wote hao walikuwa ni makasisi wa dhehebu lililojitenga kutoka kanisa la Fundamentalist Church of Jesus Christ of Latter-Day Saints (FLDS)
Bwana Blackmore alifukuzwa kutoka FLDS mwaka 2002 na mahala pake pakachukuliwa na bwana Oler.
Matawi ya dhehebu hilo yako nchini Marekani ambapo kuna wanachama karibu 10,000
Kuoa wanawake wengi ni haramu chini ya sheria za Canada, Palisi nchini Canada walianza kuchunguza dhehebuhilo mnamo miaka ya 1990.
0 comments:
Post a Comment