
Matokeo ya awali yanatarajiwa kufuatia uchaguzi wa wajumbe wa Bunge la Katiba uliofanyika nchini Venezuela kwa ajili ya kuandika Katiba Mpya.
Takriban watu kumi wameripotiwa kuuawa katika siku inayotajwa kuwa ni umwagikaji damu baada ya miezi minne ya machafuko.
Zaidi ya watu mia wamepoteza maisha yao.
Kumekuwa na mapambano kati ya polisi na waandamanaji ambao wanapinga Bunge hilo la Katiba ambapo wamekuwa wakiweka vizuizi barabarani.

Zoezi hilo liligomewa na vyama vya upinzani vinavyompinga Rais Nicolas Maduro vyenye wabunge wengi katika bunge la Venezuela.
Wanasema anataka kuendelea kungangania madarakani.
Mwandishi wa habari wa BBC nchini Venezuela anasema changamoto kubwa kwa Rais Maduro ni namna atakavyoongoza baada ya kupigwa kwa kura hiyo katika mazingira uhasama.

0 comments:
Post a Comment