Wednesday, 5 July 2017

DANTE ASHANGAZWA NA HILI LA MWANAMISI OMARY


Image result for mwanahamisi omary

Dar es Salaam. Beki wa kati wa Yanga, Andrew Vincent 'Dante'amemzungumzia staa wa Twiga Stars, Mwanahamis Omary kwamba ni mwanamke wa aina yake, kutokana na kufanya mazoezi na wanaume mitaani bila kujali usalama wake.
"Mazoezi ya mtaani hayana mwamuzi kwamba sheria zitafuata, yanatumia nguvu, kuumizana , kasi, lakini yeye anakuwa mwanamke tofauti wakati mwingine, tukicheza naye tunajisahau kwamba yeye ni jinsi tofauti anakimbiza hadi tunabakia kushangaa,"anasema
Dante anasema angekuwa nchi za Ulaya basi kipaji chake kingemfanya tajiri, kutokana ana jinsi ambavyo anajifua kwenye mazoezi na matunda yake ni msaada ndani ya kikosi cha Twiga Stars.
Anasema wakati wa mazoezi, anakusanya nyomi ya watu wanawake kwa wanaume ambao wanamshangaa kupishana vikombo na wanaume bila kuogopa na kufanya akabwe kama kawaida.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive