Monday, 24 July 2017

BOKO NA SIMBA HII KAZI IPO MAZOEZINI



 Kikosi cha Simba kimetimiza wiki moja na ushei sasa kambini Afrika Kusini, lakini utamu umezidi kunoga baada ya nyota wake waliokuwa Taifa Stars wakianza kutua kuimarisha kambi hiyo.


Simba wamejichimbia mjini Johannesburg wakijifua kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na mashindano ya kimataifa, lakini iliwakosa nyota wake waliokuwa Stars iliyotolewa na Rwanda wikiendi iliyopita katika michuano ya Chan.

Nyota waliotua Simba jana Shiza Kichuya, Mzamiru Yasin, Salim Mbonde na John Bocco 'Adebayor' wakati Said Mohamed 'Nduda' na Erasto Nyoni wakitarajiwa kujiunga leo hii.

Kipa Aishi Manula na kiungo, Mnyarwanda Haruna Niyonzima watachelewa kutokana na mchakato wa usajili wao, huku Shomari Kapombe akikwama kwa sababu ya majeraha.

Kocha Joseph Omog alisema kwa furaha; "Ujio wa wachezaji hao ni jambo zuri na itatusaidia katika maandalizi tutakayofanya, nahitaji kuwajua na kuwaona uwanjani wote na ndipo nitajua namna ya kuwatumia na ubora wa kila."

"Tutakapokuwa pamoja watapata kuzoeana na kutengeneza kikosi kilichoimara na chenye ushindani tofauti na maandalizi ya wachezaji wachache,"alisema Omog kwa furaha.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive