Mchezaji wa timu ya Azam, Erasto Nyoni.
UONGOZI wa Azam FC umewaita mezani mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga ili kuzungumza nao kuhusu usajili wa mchezaji wao kiraka, Erasto Nyoni.
Yanga wameanza kuiwinda saini ya Nyoni baada ya kocha wao, George Lwandamina raia wa Zambia kupendekeza asajiliwe kwa ajili ya kuziba pengo la kiungo mkabaji ambalo linaisumbua timu hiyo.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Ofisa Habari wa Azam, Jaffar Idd
amesema kama Yanga wana nia ya kweli ya kumtaka Nyoni basi wawafuate
mezani kwa ajili ya kujadiliana nao juu ya bei ya kuwauzia.
“Tunasikia tu kwamba nyota wetu fulani wanatakiwa na Yanga lakini
wenyewe bado hawajatufuata kwa ajili ya kuzungumza nasi kujadili bei za
kuwauzia nyota hao ambao wanawataka,” alisema Idd.
0 comments:
Post a Comment