
Siku moja baada ya kuripotiwa mauaji ya Mwenyekiti wa Kitongoji
na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mangwi kilichopo Kata ya Mchukwi
wilayani Kibiti katika Mkoa wa Pwani, IGP Simon Sirro ametembelea
kijijini hapo kutoa pole kwa wafiwa.
Aidha, IGP Sirro amewataka wananchi kijijini hapo kutowafumbia macho
wahalifu wanaotenda mauaji hayo akiwataka kushirikiana na Jeshi la
Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu hao.

IGP
Simon Sirro akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Mangwi, Kata ya
Mchukwi alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji Mwenyekiti wa
Kitongoji na Afisa Mtendaji wa Kijiji.

IGP Sirro aizungumza na Wananchi wa Mangwi alipowatembelea baada ya mauaji ya Mwenyekiti wa Kijiji na Afisa Mtendaji

IGP Sirro akitoa rambirambi ya msiba kwa Wananchi wa kijiji cha Mangwi

IGP
Sirro akikagua nyumba iliyochomwa moto na wahalifu waliofanya mauaji ya
Mwenyekiti wa Kitongoji na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mangwi. (Picha
zote na Hassan Mndeme – Jeshi la Polisi).
0 comments:
Post a Comment