Mtoto mwenye umri wa miezi minne ameibiwa katika mtaa wa ustawi wa jamii kata ya Nyamanoro wilayani Ilemela jijini Mwanza.
Imeelezwa kuwa watu waliomuiba mtoto
huyo wamemchukua mama mzazi wa mtoto huyo kwa lengo la kwenda kufanya
kazi za ndani lakini baada ya kufika Nyamanoro walimpa shilingi elfu kumi kwenda kununua mkate na baada ya kurudi amekuta tayari wameshaondoka na mtoto wake.
Wakizungumza kuhusu tukio hilo baadhi
ya wananchi wamesema kuwa jambo hilo limewashangaza kwani wameshindwa
kuelewa lengo la watu hao kumuiba mtoto huyo ni nini na kuwaomba wazazi
kuwa makini na watoto wao.
Akizungumza tukio hilo, Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Mwanza Ahmed Msangi,
amesema kuwa watu waliofanya tukio hilo mama mzazi wa mtoto anawafahamu
hivyo jeshi la polisi linaendelea na msako wa kuwatafuta watu hao.
Hata hivyo Kamanda Msangi amesema
jeshi la polisi mkoani humo linaendelea kuwasaka watu waliohusika na
kumuiba mtoto huyo na kwamba watakapobainika watafikishwa katika vyombo
vya dola.
0 comments:
Post a Comment