Wizara ya mambo ya ndani nchini Saudia inasema maafisa wa usalama wamesambaratisha njama ya shambulizi la kigaidi lililolenga msikiti wa Grand Mosque mjini Mecca.
Msemaji
wa polisi anasema mshukiwa wa shambulizi hilo alifumaniwa kwenye jengo
la makaazi ambapo alijilipua na kubomoa jengo hilo, baada ya
ufyatulianaji risasi na polisi kwa muda mfupi.
Watu 11, wakiwemo mahujaji 6 wa kigeni na maafisa 5 wa usalama walijeruhiwa.
Wizara hiyo aidha inasema watu watano akiwemo mwanamke mmoja
walitiwa mbaroni katika maeneo yanayokisiwa kuwa maficho ya magaidi
katika mji wa Mecca na Jeddah.
.Jengo hilo lilianguka na kuwajeruhi watu 11 ikiwemo maafisa wa polisi .
Washukiwa wengine watano wamekamatwa, maafisa wanasema.
Maafisa wa Saudia hawakutoa maelezo zaidi kuhusu kutibuliwa kwa shambulio hilo.
Saudia
katika miaka ya hivi karibuni imekabiliwa na mashambulio mabaya ya
mabomu mengi yakitekelezwa na wapiganaji wa Islamic State.
Mashambulio mengi yamelenga watu wa madhehebu ya shia walio wachache na vikosi vya usalama.
Manmo
mwezi Julai 2016, maafisa wanne wa usalama waliuawa katika shambulio la
kigaidi karibu na msikiti wa mtume Mohammed mjini Medina.
Saudia
ni mwanachama wa muungano wa majeshi yanayoongozwa na Marekani
yanayokabiliana na Islamic State pamoja na makundi mengine ya Kijihadi
nchini Syria na Iraq.
0 comments:
Post a Comment