Wednesday 28 June 2017

MALINZI NA MWESIGWA WANASWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA RUSHWA


Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa wameshikwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kupelekwa Polisi kwa ajili ya uchunguzi dhidi yao kwa tuhuma za rushwa.

Hilo limethibitisha na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Takukuru, Mussa Misalaba ambaye amesema taarifa zaidi wataitoa baada ya kumaliza uchunguzi wao, kwa sasa ifahamike kuwa viongozi hao wanawashikilia.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa Malinzi na Mwesigwa walipelekwa Sentro jana na leo asubuhi wamepelekwa Makao Makuu ya Takukuru kwa ajili ya uchunguzi kwa tuhuma zinazowakabili.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive