Monday, 2 January 2017

YANGA KILELENI KUNDI B MAPINDUZI CUP 2017


Bado michuano ya Kombe la Mapinduzi 2017 inaendelea katika uwanja wa Amaan, usiku wa January 2 2016 ndio siku ambayo michezo ya Kundi B ilichezwa kwa mara ya kwanza, Yanga walicheza dhidi ya Jamhuri ya Pemba katika mchezo wao wa kwanza wa Kundi B.
Yanga ambao walishusha kikosi chao kamili, walifanikiwa kuifunga Jamhuri ya Pemba goli 6-0, idadi ambayo imewafanya kuwa ndio timu ya kwanza katika michuano ya Kombe la Mapinduzi 2017 kufungwa idadi kubwa ya magoli katika mchezo mmoja.
Magoli ya Yanga yalifungwa na Simon Msuva dakika ya 19, 40, Donald Ngoma dakika ya 23, 37, Thabani Kamusoko dakika ya 59 na goli la mwisho la Yanga lilifungwa na Juma Mahadhi akitokea benchi, kwa matokeo hayo Yanga wanapata nafasi ya kuongoza Kundi B wakiwa na point 3 sawa na Azam FC ila Yanga anaongoza kwa tofauti ya goli 5.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive