Leo
January 06 2017 habari iliyoripotiwa na vyombo vya habari vya kimataifa
imeeleza kuwa mahakama mjini Nanjing, China, imewafunga jela wanaume
wawili waliowatapeli wateja kupitia benki bandia.
Watu hao
waliotambuliwa kwa majina Zeng na He, walipatikana na makosa ya
kujipatia yuan Dola milioni 63 sawa na takribani Bil 136.6 kutoka kwa
wateja 400, wamefungwa jela miaka tisa.
Imeelezwa
walianzisha chama cha ushirika ambacho ofisi yake ndani zilifanana na za
benki moja inayomilikiwa na serikali, walikuwa na madawati na makarani
wenye sare zilizofanana na makarani rasmi wa benki ya serikali. Hata
stakabadhi za kuweka amana ya pesa kwenye benki zilikuwa sawa na za
benki ya serikali.
Ingawa
taasisi hiyo ilikuwa na kibali cha kuhudumu kama chama cha ushirika,
haikuwa na kibali cha kuhudumu kama benki. Wahudumu waliwavutia wateja
kwa kuwaahidi viwango vya juu vya riba kwa pesa walizoweka amana.
Shughuli
haramu za taasisi hiyo ziligunduliwa na mfanyabiashara aliyekuwa
ameahidiwa riba ya juu alipodai riba aliyoahidiwa lakini akakosa kulipwa
na akatoa taarifa kwa maafisa wa polisi mwaka 2014 na baada ya hapo
uchunguzi wa kina ulianzishwa.
Source: BBC
0 comments:
Post a Comment