MKAZI mmoja wa kijiji cha Kalundi kilichopo kata ya Kipande wilayani
Nkasi, Vedast Kazumba (51) amejiua kwa kujinyonga kwa kile kinachodaiwa
kuwa alighadhabika, baada ya mkewe kumnyima kitoweo cha samaki mbichi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando alithibitisha tukio hilo.
Alisema ni la usiku wa mkesha wa Mwaka Mpya na kwamba Kazumba alifikia
uamuzi huo mgumu kwa kujinyonga akitumia kamba ya katani .
Alieleza kuwa hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa na polisi kuhusu tukio
hilo na uchunguzi wake unaendelea . Habari kutoka kijijini humo,
zinaeleza kuwa chanzo cha Kazumba kujinyonga ni kukasirishwa na kitendo
cha mkewe, Antoniata Mwisua kumnyima kitoweo cha samaki mbichi.
“Mke wa marehemu aitwae Antoniata alimwandalia mumewe huyo chakula cha
usiku, kitoweo chake kikiwa ni samaki mbichi alimkomba samaki huyo kisha
akamwomba amwongezee kitoweo kingine cha samaki, lakini mkewe
alimweleza kuwa kitoweo hicho kimekwisha. Ndipo mumewe alipokasirika
akidai kuwa mkewe amemnyika kwa makusudi kitoweo hicho ndipo alipochukua
hatua ya kuzira kula“ alieleza mmoja wa mashuhuda kwa masharti ya
kutoandikwa gazetini.
Akizungumzia mkasa huo , Mwenyekiti wa Kijiji cha Kalundi , John Kalasa
alidai kuwa marehemu wakati wa uhai wake alikuwa ni mtu mwenye kujawa na
ghadhabu ambapo mara kadhaa alisikika akitishia kujinyonga.
0 comments:
Post a Comment