Habari nyingine kubwa kwa Afrika sasa hivi ni Yahya Jammeh kukubali kuachia madaraka ya Urais Gambia baada ya kushindwa na mpinzani wake Adama Barrow kwenye uchaguzi mkuu uliopita.
Jammeh ameondoka kwa Ndege kwenye taifa
hilo na hii picha hapa chini inamuonyesha akiwa anaingia kwenye Ndege
na akipungiwa mikono ya byebye na baadhi ya Wafuasi wake ikiwa ni muda
mfupi baada ya Bendi ya Jeshi kutumbuiza.
Wakati wote huo Jammeh
alionekana akiwa na kitabu kitakatifu cha Koran na alitumia mkono
huohuo ulichokibeba kuwapungia waliojitokeza uwanja wa ndege kumuaga
huku ikiaminika anakwenda Guinea kwa sasa wakati akisubiri kuhamia moja
kwa moja kwenda kuishi kwenye taifa jingine.
BBC wameripoti kwamba
wakati anaondoka uwanja wa ndege Wafuasi wake na baadhi ya Wanajeshi
walionekana kuhuzunika na hata wengine kutokwa machozi lakini mitaani
wengi wamefurahia kuondoka kwake akiwa ni Rais wa kwanza wa Gambia
kuachia madaraka kwa amani toka ilipopata Uhuru mwaka 1965.
Yahya ambaye
ameiongoza nchi hiyo kwa miaka 22, saa chache baada ya matokeo
kutangazwa alikubali kushindwa lakini baadae akabadili mawazo na kusema
amehujumiwa na kwamba yeye ndio mshindi hivyo akaendelea kung’ang’ania
madaraka.
Baada ya kuendelea kung’ang’ania Mataifa mbalimbali ya Afrika yalifanya mazungumzo na ECOWAS
wakamtaka aachie madaraka ambapo saa kadhaa zilizopita kupitia
Television ya taifa akatangaza kukubali kuachia madaraka kwa amani na
asingependa kuona umwagaji damu unatokea.
Umoja wa nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS)
ulimuamuru Jammeh kuachia madaraka kabla ya saa sita mchana lakini
mwenyewe akaomba aachie madaraka ifikapo saa kumi jioni na kweli
ametekeleza.
Gambia ni miongoni mwa mataifa madogo
Afrika ambapo mpaka mwaka 2013 sensa ilikua inasema idadi ya watu ni
milioni moja na laki nane na maamuzi ya Jammeh kuachia madaraka
yalitangazwa baada ya mazungumzo na Marais wa Mauritania na Guine.
0 comments:
Post a Comment