
Mwaka 2017, utakuwa wa kihistoria nchini Norway ambapo serikali imetangaza kuanza kuzima mitambo yote inayoendesha Radio za FM kuanzia wiki ijayo na kuhamia mfumo mwingine wa kisasa zaidi uitwao Digital Audio Broadcasting (DAB), na uzimaji utafanywa kwa awamu ambazo zitakamilika rasmi mwaka 2018.
Serikali
ya Norway imesema inazima mitambo ya radio za FM na kuhamia kwenye
mfumo wa utangazaji wa digital radio unaofahamika kama DAB
utakaomuwezesha mzikilizaji kupata radio nyingi zaidi ya kulimo mfumo wa
masafa (Frequency), na pia utaongeza ubora wa sauti za radio.
“Sababu
kubwa ya kufanya hivyo japokuwa inakuwa nchi ya kwanza duniani ni
kwamba Norway ina mazingira magumu sana kwenye kusafirisha mawimbi ya
radio za FM kutokana na Jiografia yake, Norway ina mafuriko ya mara kwa
mara, milima mirefu, pamoja na jamii zilizojitenga. Hii imekuwa
ikiongeza gharama zaidi kwenye ujenzi wa mitambo ya FM ukilinganisha na
nchi nyingine” – Serikali ya Norway.
Maamuzi
haya yanaifanya Norway kuwa nchi ya kwanza duniani kuufuta kabisa mfumo
wa utangazaji wa radio za FM na kuhamia mfumo wa matangazo ya
kidigitali, ikiwa ni maamuzi yaliyopitisha na bunge la nchi hiyo siku
chache zilizopita.


Pamoja
na kupitishwa sheria ya kuzima radio za FM nchini humo, umefanywa
utafiti kuhusu jinsi wananchi walivyolipokea suuala hilo ambapo kwa
mujibu wa kura zilizopigwa imeonesha kuwa 66% ya wananchi wameupinga
uamuzi wa serikali kuzima mfumo wa FM, wakati 17% wamekubali.
Inaelezwa
kuwa baada ya Norway kuzima mitambo ya FM, nchi nyingine zitakazofata
ni pamoja na Switzerland ambayo imetangaza kuzima radio za FM ifikapo
mwaka 2020, Uingereza na Denmark zimepanga kuhama mfumo huo pia. Nchi
nyingi zinasubiri kitakachotokea baada ya Norway na endapo utakuwa mfumo
rahisi na mzuri zaidi nyingi zimeonesha kuwa zitahamia mfumo.
Ikumbukwe
hapa Tanzania ilitokea wakati Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
ilipotangaza kuzima mitambo ya analogy iliyokuwa inaendesha utangazaji
wa Televisheni ambapo mpaka sasa ni nchi nzima imeshakamilisha mfumo huo
na kuingia kwenye utangazaji wa Digital Visual Broadcasting (DVB
0 comments:
Post a Comment