Saturday, 31 December 2016

HATIMAE MWAROBAINI WA RAIS KABILA NCHINI CONGO WAPATIKANA


Baada ya muda wa utawala wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Joseph Kabila kumalizika mwezi huu lakini kutong’atuka kwake kulisababisha maandamano yaliyokumbwa na ghasia ambapo watu zaidi ya 40 waliripotiwa kufariki.
Habari iliyoripotiwa na BBC leo December 31 2016 imesema kuwa wapatanishi wanaojaribu kutatua mzozo wa kisiasa huko Jamhuri ya Kidemocrasi ya Congo wamesema serikali ya nchi hiyo na vilevile washirika kutoka makundi ya upinzani sasa wamefikia muafaka.
Maaskofu kutoka kanisa katoliki waliokuwa wakiendesha kikao hicho cha majadiliano wanasema makubaliano ni kwamba rais Joseph Kabila anaweza kusalia madarakani kwa muda wa mwaka mmoja, lakini ni sharti uchaguzi ufanyike ndani ya kipindi cha miezi 12.
Sharti jingeni ni kuwa Rais Kabila asiwanie tena kiti cha urais katika uchaguzi huo. Mwafaka huo unatarajiwa kutiwa saini hii leo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive