
Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno na mshambuliaji wa Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo ameamua kuonesha mapenzi wa dhati kwa mashabiki wake kwa kuanzisha application yake ya kupiga selfie nae bila kuonana ana kwa ana.
Application hiyo inayotumia jina la kibiashara la staa huyo inaitwa CR7 Selfie inapatikana katika play store tayari na gharama ya kununua application hiyo ni dola 2.22, lengo la Ronaldo kuanzisha application hiyo ni kuchangisha pesa kwa ajili ya watoto wakimbizi.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri brand ya Cristiano Ronaldo inazidi kukua siku hadi siku, Ronaldo tayari
ameingia katika masuala ya fashion na brand hiyo, mavazi ya kuogelea na
biashara za hotel ambazo zote zinatumia jina hilo hilo la CR7.
0 comments:
Post a Comment