
Kiungo wa Ufaransa aliyekuwa akichezea klabu ya Juventus ya Italia Paul Pogba August 8 2016 aliwasili katika klabu ya Manchester United kwa ajili ya kukamilisha usajili wake utakaovunja rekodi ya mchezaji wa Real Madrid Galeth Bale mchezaji aliyesajiliwa kwa dau kubwa na kuweka rekodi ya Dunia.

Pogba akielekea katika uwanja maarufu jijini manchester AON ambao Timu ya Manchester United utumia kwa ajili ya mazoezi akiwa ndani ya gari nyekundu aina ya Chevrolet Camaro(iliopo mbele mstari wa katikati) kwenda kufanya vipimo vya afya ili aweze kukamilisha usajili wakeya kufanya vipimo vya afya na kukamilisha usajili wake.

Kiungo huyo ambaye aliondoka Manchester United mwaka 2012 kwa ofa ya pound 800,00 anatajwa kuwa atasaini mkatab wa miaka mitano wa kuitumikia Manchester United kwa ada ya usajili ya rekodi ya dunia ya pound milioni 110, mkataba na Manchester United utamuwezesha kuingiza mshahara wa pound 290,000 kwa wiki.

Paul Pogba akiwa safarini kuelekea katika jiji la Manchester


Yeo Moriba mama mzazi wa Paul Pogba alivyowasili katika uwanja wa mazoezi wa Manchester United
0 comments:
Post a Comment