Home »
» JPM - BINADAMU WOTE NI WAMOJA
RAIS
John Magufuli amesema kwamba binadamu wanapaswa kuwa wamoja hata kama
wana tofauti mbalimbali zikiwamo za kimadhehebu ya dini, siasa na kanda,
huku akiwaomba viongozi wa dini kuendeleza juhudi zao za kuliombea
taifa na kuwaunganisha wananchi licha ya tofauti walizo nazo.
Dk Magufuli alitoa kauli hiyo jana
baada ya kumalizika kwa Misa Takatifu ya kuadhimisha Jubilee ya miaka 50
ya Ndoa ya Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na mkewe, Anna
iliyofanyika kwenye Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini
Dar es Salaam jana.
Hafla
ya Jubilei hiyo ilifanyika nyakati za mchana kwenye Ukumbi wa Kardinali
Rugambwa, uliopo kando ya Kanisa la Mtakatifu Petro-Oysterbay na
ilitanguliwa na Misa ya shukrani, iliyofanyika katika kanisa hilo majira
ya asubuhi.
Jubilei hiyo ilihudhuriwa na viongozi
mbalimbali wakiwemo Rais Magufuli na mkewe, Mama Janeth , Makamu wa
Rais, Samia Suluhu Hassan, Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete,
Rais mstaafu wa Awamu ya Sita wa Zanzibar, Dk Amani Abeid Karume, Mke
wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, mawaziri wakuu wastaafu Cleopa
Msuya, Dk Salim Ahmed Salim, Jaji Joseph Warioba na Edward Lowassa.
Misa Takatifu ya Shukrani iliongozwa na
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Askofu Josephat Lebulu na
kuhudhuriwa na maaskofu na maaskofu wakuu saba, akiwemo Askofu Mkuu wa
Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
0 comments:
Post a Comment