Habari
mpya mjini kwa sasa ni kuwa wale mahasimu wawili wa muda mrefu,
Blandina Chagula ‘Johari’ na Chuchu Hans ambao ni mastaa wenye majina
makubwa katika kiwanda cha filamu nchini, wamemaliza tofauti zao na sasa
ni mashostito wakubwa, Risasi Mchanganyiko lina ubuyu mzima.
Chanzo
cha kuaminika kililiambia gazeti hili kuwa, mabinti hao ambao sababu ya
bifu lao linatajwa ni kumgombea kimapenzi Vincent Kigosi ‘Ray’ ambaye
pia ni muigizaji, hivi karibuni walionekana wakiwa wamekaa pamoja katika
Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es Salaam na wakati mwingine
wakiitana chemba walipozungukwa na watu.
johari2“Niaje
mdaku? Ninakumegea ubuyu kwamba Johari na Chuchu hivi sasa ni mashosti
ile mbaya, kwa macho yangu nimewaona pale Leaders wakibadilishana
mawazo, tukapigwa na bumbuwazi. Tumeambiwa kuwa kazi yote hiyo imefanywa
na Steve Nyerere,” chanzo chetu kilitiririka.
Baada
ya kuunyaka ubuyu huo, gazeti hili lilianza na Chuchu ambaye simu yake
iliita bila kupokelewa, lakini kwa upande wake Johari alipotakiwa
kuidadavua ishu hiyo, aliishia kucheka na kudai hataki kuongelea mambo
hayo.
“Mmh
jamani nani kakwambia hiyo habari, mmeshaanza mambo yenu, mimi sitaki
kuongelea hizo ishu, achana nazo bwana,” alisema Johari huku akiangua
kicheko.
Ili kuweka mambo sawa, Steve Nyerere, Mwenyekiti wa zamani wa Bongo Muvi alipatikana kupitia simu yake ya mkononi;
“Ni
kweli hawa wasanii hivi sasa wamemaliza tofauti zao, kwani wewe huoni
kama hili ni suala la heri au hukutaka wapatane? Hiki ni kitu cha
kumshukuru Mungu. Kuhusu kuwapatanisha hilo mimi sijui, ila wewe elewa
tu kuwa hivi sasa wanaelewana mno.”
Awali,
Johari alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Ray, uliosababisha wawili
hao kuanzisha kampuni yao inayojishughulisha na mambo ya filamu ya RJ
Company, lakini ghafla Chuchu Hans alianza kuonekana akiwa na ukaribu na
mwanaume huyo, kitendo kilichosababisha kuwepo na kutokuelewana kati
yao kulikodumu kwa muda mrefu.
Chanzo:Global Publishers
0 comments:
Post a Comment