Programu ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp ipo mbioni kuongeza sehemu mpya nne ambazo zitawasaidia watumiaji wake kupata unafuu na urahisi wakati wa kutumia.
Taarifa kutoka kutoka kwenye mitandao mbalimbali ya Teknolojia duniani zinasema kuwa WhatsApp inafanyia kazi sehemu kubwa nne ikiwemo ya kubadilisha na kuhaririri ujumbe uliyomtumia mlengwa kabla hajausoma, sehemu hii itafanya kazi pale ambapo meseji hiyo itakuwa haijapokelewa kwa kuweka tiki mbili za blue.
Maboresho mengine ni kucheza moja kwa moja kwa video za Youtube ndani ya Programu ya WhatsApp, Kurudisha meseji, picha au video ulizotuma kwa muhusika, kwa wazoefu wa mtandao wa WhatsApp au watu walioanza kutumia tangia mwaka 2015 sehemu hii ilionekana kwenye Whatsapp beta kabla ya kuondolewa mwaka jana 2016, Sehemu hii itarudishwa tena ambapo mtu atapata dakika 5 za kurudisha meseji, Jumbe, picha au video alizotuma kimakosa.
Kwa mujibu wa mtandao wa WABETA Info umeripoti kuwa kabla ya mwezi Septemba mwaka huu, Programu ya WhatsApp ambayo inatumiwa na watu zaidi ya Bilioni 1 duniani itatangaza mabadiliko hayo.
0 comments:
Post a Comment