Ghetto Kids wakiweka pozi.
Moyo wa subira, juhudi na ubunifu ndiyo
kila kitu katika maisha ya mtu mwenye shauku ya mafanikio. Hicho ndicho
kilichowafikisha watoto wa Ghetto Kids
kwenye kilele cha mafanikio barani Afrika na duniani. Kwa sasa watoto
hawa wameula, wanaogelea kwenye fedha. Dunia inawajua na wana mvuto wa
kipekee wanapokabidhiwa jukwaa kufanya mambo.
Ghetto Kids, hatari.
KAMA UTANI VILE
Ghetto Kids walianza kuonekana kama
utani vile kwenye mitandao ya kijamii wakicheza muziki kwa staili ya
aina yake kwa kutumia Wimbo wa Maria Rosa wa mwanamuziki, Eddy Kenzo wa
Uganda, tena kwa staili ya kuchekesha na kivituko zaidi.
Walikuwa wakicheza muziki wa video kali
zilizotoka na zilizoonekana kuwashika mashabiki wengi duniani, hasa kwa
kuzingatia jina la mwanamuziki husika aliyeachia ngoma yake.
Ghetto Kids wakiwa na French Montana.
COVERS ZA NGOMA KALI
Mbali na kufanya covers (kurudia video
za nyimbo kwa staili tofauti) za video za Kenzo pia walifanya za ngoma
kali za mastaa wakubwa duniani kama Sorry ya Justin Bieber, Make Am ya Patoranking na nyingine kibao huku wakitamaniwa na mastaa wengi kama Nicki Minaj na French Montana aliyediriki kusema kuwa wanajua kucheza zaidi ya Chris Brown.
Nikiri kuwa, nilipoona video zao kwa
mara ya kwanza kwenye mitandao ya kijamii, nilivutiwa na staili yao hiyo
ya kucheza muziki mitaani kwa mpangilio wa aina yake, wakionekana
wachafu kwa kujigaragaza kwenye mavumbi na matope.
Ghetto Kids.
MAISHA HALISI
Kilichonivutiwa zaidi kwa watoto hawa
ni namna walivyoakisi mazingira ya Kiafrika na maisha halisi ya sehemu
kubwa ya bara hilo. Mavazi yao yanayowaonesha kama vile wanatoka familia
zisizokuwa na uwezo kiasi cha kuvaa mavazi yaliyochanika na kuwekewa
viraka kuonesha maisha ya familia nyingi ambazo hazina uwezo wa
kuwanunulia watoto wao nguo mpya.
Ghetto Kids wakiwa katika picha ya pamoja.
GETTO KIDS NI AKINA NANI?
Kadiri siku zilivyosonga ndivyo
walivyozidi kuwa gumzo mitandaoni. Hapo ndipo nilipopata shauku ya
kutaka kujua Getto Kids ni akina nani?
Jina kamili la kundi lao ni Triplets Ghetto Kids kutoka nchini Uganda. Kundi hilo linaundwa na watoto ambao wote wamezaliwa baada ya mwaka 2000 (yupo aliyezaliwa 2010). Baadhi yao ni pamoja na Ada, Patricia, Ashley, Man King, Ronnie, Isaac, Fredy, Nyangoma, Kokode na wengineo. Mwaka 2014 walipata pigo la kufiwa na mwenzao kwenye ajali ya baiskeli aliyeitwa Alex.
Patricia.
WANAMILIKIWA NA EDDY KENZO
Kwa mujibu wa mwanamuziki wa Uganda anayelimiliki kundi hilo, Eddy Kenzo, watoto hao aliwakusanya mitaani wakiwa hawajuani.
Wengi wao ni watoto waliokulia maisha
magumu ya mitaani kutokana na familia zao kutokuwa na uwezo wa
kuwapeleka shuleni au kuwapa malezi bora. Pia baadhi yao ni yatima.
Kenzo anasema kuwa, tangu kuanza kwa
safari yao ya ku-dance mavumbini na kwenye matope, walionekana watoto wa
mitaani wasiokuwa na mwelekeo wa kimaisha.
Eddy Kenzo.
KENZO AONA TOBO
Ilibidi kutumia staili hiyo baada ya
kubaini kuwa, kuna tobo au mwanya ambao wengi hawauoni. Kwamba, staili
hiyo inaakisi uhalisia wa familia zilizo nyingi za Kiafrika na kwamba
ingepata mvuto kwa sababu ni staili ya kipekee.
Kenzo ni mwanamuziki mkubwa nchini
Uganda hivyo anasema si kweli kwamba alishindwa kuwapiga sopusopu na
pamba kali za kisanii, lakini alitaka waonekane hivyo kuleta utofauti na
ndiyo maana wakiwa nje ya steji au kazi yao hiyo wanaonekana ni watoto
wa matajiri flan.
WAPENYA ULAYA, MAREKANI
Mdogomdogo, Ghetto Kids walianza
kuiteka Uganda, Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla. Baadaye walivuka
mipaka ya Bara la Afrika. Wakaanza kulamba shoo mabara mengine,
wakialikwa kwenye matamasha makubwa ya Ulaya na Amerika (Marekani).
Sasa maisha ni bomba. Wanatamba hadi
Hollywood, Marekani. Mwaka huu walipafomu kwenye moja ya steji kubwa za
kimataifa na kutumbuiza mbele ya umati mzito wenye macho ya wasanii
wakubwa na watu mashuhuri duniani kwenye tuzo kubwa za BET za Marekani.
French Montana.
FRENCH MONTANA AWAONA
Katika harakati zao hizo, walionekana
na staa mkubwa wa muziki wa Marekani, French Montana. Staa huyo
alipowaona watoto hao, aliamua kuwatumia katika tour (ziara za kimuziki)
sehemu mbalimbali duniani.
Mbali na hilo, pia wamekuwa wakipata coverage (kuandikwa) kwenye majarida makubwa ya burudani kama Vibe la Marekani.
French Montana amewatumia pia kwenye
video ya ngoma yake kali ya Unforgettable aliyomshirikisha Rapa Swae Lee
ambayo imetazamwa na zaidi ya watu milioni 170 kwenye Mtandao wa
YouTube.
DOLA LAKI 1 KUWASAFIRISHA
Kupitia Jarida la Vibe, French Montana
anasema kuwa, baada ya kuwaona watoto hao kwenye mitandao ya kijamii,
alitumia kiasi cha dola laki moja (zaidi ya Sh. milioni 220)
kuwasafirisha kutoka Uganda hadi Marekani kwa ajili ya kuwatumia kwenye
kazi zake za kisanaa.
“Stori yao ni ya aina yake, jinsi
walivyokutanishwa na namna wanavyoishi pamoja,” anasema French mwenye
asili ya Morocco na kuongeza;.
“Unforgettable (ngoma yake) haikuwa
ngoma yangu pekee. Nilipenda kuwaona watoto hawa wakiwa na furaha.
Ukweli ninapenda kuwaona sasa wana furaha.”
0 comments:
Post a Comment