Saturday, 20 August 2016

SABABU ZINAZOPELEKEA KUZIMWA KWA SIMU PINDI NDEGE INAPOTAKA KUTUA AMA KUPAA

By Denis Massawe

Najua kama ni mtumiaji wa usafiri wa ndege utakuwa ushasikia taratibu za abiria kuzima simu wakati ndege inapotaka kupaa au kutua. 

Ila huenda hukawa hujui sababu zinazo pelekea  kufanya hivyo, inawezekana ulishajiuliza usipozima unaweza kusababisha ndege kupata ajali au? jibu ni Hapana, isipokuwa unaweza kusababisha muingiliano wa mawasiliano kati ya rubani na waongozaji.

Vibrations au miungurumo ya simu na vifaa vingine vya electronics vinahusika kwa kiasi kikubwa kuvuruga mawasiliano mazuri kati ya rubani na wanaomuongoza, hivyo huwa tunashauriwa kuzima simu na vifaa vingine vya electronics wakati wa kupaa na kutua kwa ndege. Hiyo ni moja kati ya sababu kuu zilizotajwa juu ya swali la ”Kwanini tuzime simu wakati ndege inaporuka na kutua”?.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive