Thursday, 18 August 2016

LISTI YA WACHUNGAJI 10 MATAJIRI DUNIANI 2016

1. ASKOFU DAVID OYEDEPONIGERIA ($150 Million)

Askofu David Oyedepo anamiliki utajiri unaofikia dola million 150 ambayo ni zaidi ya Bilioni 300 za kitanzania  na ndio mwazilishi ya huduma ya Living Faith World Outreach iliopo Sango Otta, Ogun State, nchini Nigeria.

Askofu Oyedepo ni mtumishi wa mungu mwenye mafanikio makubwa sana miongoni mwa vitega uchumi anavyomiliki  ni meli mbili za abiria ,nyumba zilizopo Marekani na Uingereza, shule za chekechea na msingi zilipo maeneo mbalimbali ulimwenguni zenye jina la Kingdom Heritage Schools and Faith Academy respectively, makampuni ya uchapishaji na mali nyingine nyingi. 

Oyedepo  pia ni mhadhini wa vyuo vikuu viwili cha  Covenant na Landmark.     

 
2.     CHRIS OYAKHILOME - NIGERIA ($50 Million)

Pastor Oyakhilome anamiliki utajiri unafikia dola milioni 50 ambayo ni  zaidi ya Bilioni 100 za kitanzania.

Oyakhilome ndiye mwazilishi wa huduma ya Christ Embassy yenye matawi Nigeria, South Africa, England, Canada na Marekani kwa mujibu wa jarida la Forbers.

 

3. BENNY HINNMAREKANI ($42 Million)

Benny Hinny anamiliki dola milioni 42 ambayo ni zaidi ya Bilioni 91 za kitanzania.

Hinny ni muhubiri  maarufu sana, uhandaa mikutano mikubwa katika miji  mbalimbali Duniani ijulikanayo kama “Miracle Crusades”.    

 

4. CREFLO DOLLAR – MAREKANI ($27 Million)

Creflo Augustus Dollar anamiliki dola milioni 27 ambayo ni zaidi ya  Bilioni 58 za kitanzania.

 Dollar ni Mwazilishi wa huduma ya non denominational world changers church, iliopo Georgia, Marekani na huduma ya Creflo Dollar Ministerial Association.

 

5. BILLY GRAHAM MAREKANI ($25 Million)

Bill Graham anamiliki utajiri upatao dola million 25 ambayo ni zaidi Bilion 54 za kitanzania.

 

6. T.D JAKESMAREKANI ($18 MILION) 

Thomas Dexter maarufu T.D Jakes anamiliki utajiri uanaokisiwa kuwa ni dola million 18 ambayo ni zaidi ya billion 39 za kitanzania.

T.D Jakes ni mchungaji wa kanisa la The Potters House lenye washirika 30,000 lililopo Dallas, Marekani.

 

7. T.B. JOSHUANIGERIA ($15 MILION)

Temitope Balogun Joshua, maarufu T.B. Joshua anamiliki utajiri unakisiwa kuwa ni dola milioni 15 ambazo ni zaidi ya bilioni 32 za kitanzania.

 Nabii T.B. Joshua ndie muchungaji alieshika nafasi ya tatu ya wachungaji matajiri Nigeria kwa mujibu ya jarida la Forbes. 

 

8. MATHEW ASHIMOLOWNIGERIA ($10 MILION)

Mathew Ashimolow ni mchungaji kiongozi wa kanisa la Kingsway International christian Centre lililopo London.

Ashimolow anamiliki utajiri unaofikia dola milioni 10 ambazo ni zaidi ya bilioni 21 za kitanzania.

Ashimolow anamiliki vitega uchumi mbalimbali ikiwemo vituo vya radio na runinga.

9. CHRIS OKOTIE NIGERIA ($10 MILION) Okotie uatajiri wake ni dola milioni 10 ambazo ni zaidi ya bilioni 21 za kitanzania.

Okotie alipata mafanikio makubwa miaka ya 1980 alipokuwa mwanamuziki wa pop.

 

10. JOSEPH PRINCE – SINGAPORE ($5 MILION)

Prince anautajiri unaofikia dola milioni  5 ambazo nizaidi ya bilioni 10 za kitanzania.

Prince ni mwazilishi na ni mchungaji kiongozi wa kanisa la New Creation lililopo Singapore, na ni moja kati ya makanisa makubwa sana huko Asia.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive