Home »
» JE MTOTO WA OBAMA ANAFUATA NYAYO ZA BABA YAKE?

Katika moja ya hotuba zake Rais Obama
mwaka 2014 alizungumza kuhusu suala la uvutaji wa bangi ambapo alisema
kuvuta bangi ni salama zaidi kuliko kunywa pombe lakini akawasisitizia
mabinti zake kwamba hilo sio wazo zuri pia ambapo kwa mujibu wa gazeti
la The Mirror, limewahi kumuandika Obama akieleza kuwa anaamini uvutaji
bangi hauna madhara au athari za hatari kwa mtumiaji binafsi.
Pia kwa mujibu wa historia imeandikwa
kuwa Rais Obama aliwahi kuvuta bangi enzi za ujana wake, ambapo
amenukuliwa akisema kuwa “uvutaji sio kitu ambacho nachochea kifanyike,
tambua ni upotezaji muda na inaathiri afya, bangi imehalalishwa kwenye
miji ya Colorado na Washington kwa kura ya maoni na ilikuwa ni muhimu
kwa ajili ya mataifa kumaliza uhalifu wa vijana wadogo wanaotoka kwenye
familia zenye asili ya umasikini”.
Hivi karibuni familia ya Rais huyo
ambaye yuko mbioni kumaliza muda wake imekumbwa na mambo mbalimbali
ikiwemo kusambaa kwa video ya mtoto wake Malia Obama akikatika katika
moja ya tamasha nchini humo.
Tukio lingine kumuhusu binti huyo ni
kuhusishwa na uvutaji wa bangi, Inasadikiwa Malia alivuta sigara hiyo
‘haramu’ kwenye tamasha la lollapalooza kwenye Jiji la Chicago, jimbo la
Illinois ambalo ni jimbo la nyumbani kwa Rais Obama, Mmoja wa
wahudhuriaji wa tamasha hilo Jerrdin Selwyn mwenye umri wa miaka 18
alidai kuwa alimkuta Malia akiwa anavuta ganja na marafiki zake na
hakukuwa na shaka ya hilo kwani harufu ya bangi ilikuwa wazi. “Kulikuwa
na kijana mmoja pale ambaye alikuwa anavuta na akampasia Malia ambaye
alishikilia kama kwa dakika moja kisha akampatia mtu mwingine” alidai
binti huyo. Na alidai pia kuwa alikuwa na picha zinazoonesha mtoto huyo
wa Rais wa Marekani akivuta bangi hiyo.
Matukio
hayo ya mtoto huyo wa Rais kinara yanazidi kuichafua familia hiyo kwani
wengi waliamini, familia yake ingekuwa mfano wa kuigwa ikizingatiwa
kuwa Rais huyo amewahi kutaja madhara ya matumizi ya bangi katika moja
ya hotuba zake.
0 comments:
Post a Comment