
utafiti mpya wa hivi karibuni umeibuia mapya baada ya kubainika kuwa ulaji mzuri wa chocolate unaweza kuongeza uwezo wa kufikiri na hivyo kutoa fursa kwa watoto kufanya vizuri darasani.
Aidha,
utafiti huo umebaini vilevile kuwa ulaji wa chocolate husaidia kupunguza
kasi ya kawaida ya kuzeeka kwa walaji itokanayo na kuongezeka kwa
umri. Ripoti ya utafiti huo ilitolewa hivi karibuni, inabebwa na utambulisho usemao ‘ulaji
wa chocolate huongeza utendaji kazi wa ubongo” na kwamba ”unaweza
kusaidia mtu kutozeeka haraka licha ya umri kuzid kumtupa mkono’
Utafiti
huo uliochapichwa mwezi huu katika jarida la Appetite, umebaini kuwa
kumbukumbu na uwezo wa kufikiria ufumbuzi wa mambo magumu kuwa katika
kiwango cha juu kwa watu wanaokula chocolate kwa wingi. Matokeo hayo
yameripotiwa kutoathiriwa na umri wa mlaji, uzito wa mwili wala aina
nyingine za ulinganifu wa jumla wa kiafya .
Inaelezwa
zidi kuwa utafiti huo unaonyesha kuwapo kwa uhusiano mkubwa kati ulaji
wa kila mara wa chocolate na matokeo ya majaribio kuhusu uwezo wa
uubongo katika kufikiri hata hivyo utafiti huo haujathibitishwa kwa
asilimia 100 juu ya uhakika wa kisayansi juu ya kile kilichobainishwa.
Aidha
imeonekana watu wanotumia zaidi chocolate walikuwa na lishe bora zaidi
na pia kunywa pombe kwa kiasi kidogo, na makundi yote yalitegemea uwezo
wa kukumbuka mambo kupitia kiwango chao cha ulaji wa Chocolate.
SOURCE: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment