BY Denis Massawe
Tukio la kuwawa kwa Askari Polisi wanne katika shambulio lililofanywa na
watu wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi usiku wa August 23 2016
zimeendelea kuchukua headline ambapo safari hii Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi Mwigulu Nchemba alifika eneo la tukio ambapo pia Ayo TV ilipata
nafasi ya kufanya naye mahojiano.Waziri Nchemba amesema…
’Kumetokea shambulio la uvamizi lenye nia ya uovu ambalo limeua askari wanne, vijana wamefika na wataendelea na msako kuhakikisha wahalifu wote wametiwa nguvuni‘
‘Tukio lilitokea majira ya saa moja na nusu usiku ambapo bado uchunguzi unaendelea na taarifa kamili itatolewa na Jeshi la Polisi, kifupi ni kwamba shambulio lilifanywa kwa kutumia usafiri wa pikipiki na niwakati vijana wakibadilishana lindo lakini niwahakikishie wananchi kuwa watuhumiwa wote watatiwa hatiani‘ –Waziri Mwigulu Nchemba
0 comments:
Post a Comment