Home »
» TCRA WASISITIZA KUZIMA SIMU FEKI
Ikiwa imebaki miezi miwili kuzimwa kwa
simu bandia Mamlaka ya mawasiliani nchini Tanzania TCRA, imewataka
watumiaji wa simu kuhakikisha kuwa simu wanazotumia ni halisi ili
kuepukana na hofu ya madhara yatokanayo na bidhaa bandia. Mkurugenzi
Mkuu wa TCRA, Dkt. Ali Yahya Simba, amesema hayo alipokutana na
waandishi wa habari Mjini Dodoma, kwa lengo la kueleza manufaa ya mfumo
rahisi wa namba ya utambulisho kuelekea june mwaka huu ambapo simu zote
bandia zitazimwa.
Dkt.Simba amesema kuwa wameamua
kuchukua hatua kutokana na kushindwa kuzidhibiti simu hizo kutokana na
mtu wa mtandao mmoja akifanya uhalifu na akibadilisha mtandao kwa simu
ile ile anashindwa kupatikana kirahisi huku akisisitiza zoezi hili
litafanyika tarehe 16 mwezi 6 mwaka 2016.
Kwa Upande wake Meneja mawasiliano na
mahusiano ya Umma wa TCRA, Inocent Mungi,amesema kuwa uwezekano wa simu
hizo zikawa na madhara mengine ya kiafya, pamoja na utambuzi wa watu
wanaozitumia kwa uhalifu.
Nae mwanasheria mwandamizi katika
kitengo cha udhibiti na uzuiaji wa bidhaa bandia ya tume ya ushindani,
Khadija Sijaona, amesema kuwa wanaokiuka maelekezo ya tume na mamlaka ya
mawasiliano watachukuliwa hatua kali.
0 comments:
Post a Comment