Sunday, 3 April 2016

Sijawahi Kutoka na Nisha na Wala Hajawahi Kuwa Hata Mshikaji Wangu -Baraka de Prince


Msanii Baraka de Prince ambaye kwa sasa anafanya poa na ngoma yake ya 'SIWEZI' na ambaye amedondoka kwenye penzi la msanii mwenzake Najma Datan amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake yeye hajawaji kutoka kimapenzi na msanii wa filamu

Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live, Baraka de Prince alisema kwamba yeye hajawahi hata kuwa na ushikaji na msanii huyo na kusema kwamba inawezekana ni shabiki mzuri wa kazi zake ila hajawahi kutoka nae kimapenzi kama ambavyo inazungumzwa mtaani na kama ambavyo msanii huyo alivyowahi kusema kuwa anatoka na Baraka de Prince.

Mbali na hilo Baraka de Prince alizungumzia juu ya show kubwa ambayo ataifanya siku ya kesho Jumapili pale Coco Beach kwenye show iliyoandaliwa na East Africa Radio kwa ajili ya kushererekea miaka 17 toka imeanzishwa. Ambapo Baraka de Prince amesema ni show yake ya kwanza kubwa kufanya hivyo amejipanda kuwapagawisha wana ambao watatokea,

Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive