Watayarishaji wa tamasha kubwa la hiphop la Back to the City
nchini Afrika Kusini wameshangazwa na sababu za AKA kukataa kufanya
show kwenye tamasha hilo siku chache baada ya kauli kali ya Aka kusamba
mitandaoni.
AKA alisema “Sipendezwi na jinsi
watayarishaji wa matamasha Afrika kusini wanavyofanya kazi na wasanii wa
nyumbani, hata Mimi ni msanii wa kimataifa na nataka kufanyiwa na
kuchukuliwa sawa na wasanii wa kigeni mnaowaita wasanii wa kimataifa na
ndio maana sitafanya show kwenye Back To The City“.
Aka pia amekata kufanya show hio kutokana na misingi yake kuwa
alitaka kutangazwa kama wanavyotangazwa wasanii wa kimataifa wanaokuja
kufanya show hio kama Elzhi wa kundi la Slum Village kutoka American.
Pia AKA alitaka show tofauti yenye Bendi, Fataki, mfumo bora wa Taa
na muda zaidi wa kufanya show kitu ambacho kimekuwa na mvutano mkubwa
kati yake na waandaji wa tamasha hili.
0 comments:
Post a Comment