Thursday, 24 March 2016

Habari 8 kubwa kwenye TV za Tanzania March 23 2016

Kama ulikosa time ya kuangalia taarifa ya Habari ya March 23 2016 usijali millardayo.com inakupa fursa ya kuziangalia Habari nane kubwa kupitia TV za Tanzania.
Habari kutoka Channel 10Ahadi Ya Mamilioni Ya Rais Magufuli Vijijini
Baada ya kufunga kikao cha bodi ya Barabara Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, amesema ‘Hizi pesa ni za mikopo lakini sahivi mnatakiwa kuangalia ni jinsi gani hizi pesa  zitakuwa na matokeo gani katika Halmashauri zenu‘>>>Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
20160323_191203
Habari kutoka ITV...Wizi wa Mafuta Ya Ndege
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Masauni Hamad Masauni amewasimamisha kazi watumishi waliokutwa na madumu 10 ya mafuta ya ndege wakiwa na gari ya Serikali,
Ukishachukua mafuta ya ndege alafu ndege inaanguka inauwa watu alafu kumbe  wewe ni Askari wa zima moto au Askari Polisi sasa hawa nawaasimamisha kazi mara moja na hatu kali za kisheria zitafuataNaibu Waziri wa Mambo ya Ndani Masauni Hamad Masauni
20160323_201907
Habari kutoka ITVDawa Bandia Za Mimea
Wakaguzi wa viuatilifu wakamata shehena ya Dawa bandia za mimea Mlimbana na kukutwa na hatia ya kuajiri watoto wenye umri chini ya miaka 15.
Viuatilifu kama hivi kuviweka juani ni makosa makubwa sana alafu mtoto mdogo kama huyu kumuweke hapa kwa ajili ya kuuza sumu kama hii  bila kinga sio vizuri>>>Wakaguzi 20160323_201437
Habari kutoka Star TVKujiunganishia  Umeme Kinyemelezi
Meneja wa Shirika la Umeme Mwanza Mwandisi Sara Aseyi amewaambia watu wanaojiusisha na kujiunganishia Umeme kinyume cha sheria waache mara moja kwani zoezi Hilo ni endelevu ‘Wateja wa Milimani nawaambia waache wizi mara mojaMwandisi Sara Aseyi
20160323_200859
Habari kuyoka Star TV…Tuhuma Za Uhalifu
Polisi Kilimanjaro washikilia Watu 24, kufuatia na tukio lilotokea  jana saa tatu usiku maeneo ya kijiji cha Kombo Wilayani  Moshi Vijijini
Mtu anayeitwa Linda Malisa alijeruhiwa kwa kupigwa na risasi sehemu ya mguu wa kulia  kwenye ugoko na tumboni na Askari waliokuwepo kwenye oparesheni ya kuua Mbwa na  katika msako huo wahamiaji 19 kutoa Ethiopia walikamatwa‘>>>ACP Wilbroard Mtafungwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro.20160323_201236
Habari kutoka TBC1Serikali Ya Zanzibar Yaombwa Kuwapa Kipaumbele Wazee Katika Afya
Tuseme tu kwamaba raia wote wa Zanzibar wako sawa wawe wa CCM, CUF na Vyama vingine na watapewa  ulinzi sawasawa kabisa hakuna ubaguzi na hii hali ya doria  ilihimarishwa tu kama tahadhari na tahadhari hii itapungua pale tutakapo hakikisha hakuna hali yeyote ya uhalifu‘>>>.Charles Kitwanga Waziri wa Mambo ya Ndani Ya Nchi
20160323_200526
Habari kutoka TBC1...Waziri wa Nishati na Madini Apokea Taarifa ya Kamati Iliyochunguza Malalamiko
Waziri Muhongo ameyasema hayo baada ya kupata taarifa aliyoipata kutoka kwenye kamati alaiyoiunda kwa ajili ya kuchunguza malamiko ya wananchi wa nyamongo wanaouzunguka Mgodi wa Dhahabu wa North Mara
Yaliyoko huku sio ya wana kamati yaliyoko huku wamekusanya maoni kutoka kwa Wananchi, wamiliki wa Migodi na kutoka kwa Viongozi wa ngazi mbalimbali na hatakaye yakataa haya na sisi tuta mkataa‘>>>Prof: Sospeter Muhongo Waziri wa Nishati na Madini
20160323_201241
Habari kutoka Azam TWOMakonda: Hatutorejesha Baadhi ya Silaha
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amesema hawatarejesha baadhi ya silaha ‘Lakini kuna wengine wazazi wao wametangulia mbele za haki kwahiyo mimi sidhani kuwa kwenye Mirathi unaweza ukaandikiwa urithi silaha kama bunduki‘>>>Paul Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
20160323_201605
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive