![]() |
Diego Costa |
Diego
Costa amekataa kwenda kwa mkopo katika timu za SIPG na Tianjin Quanjian
za China ambapo angelipwa pauni milioni 13 kati ya sasa hadi mwezi
Novemba. (Sun)
![]() |
Danny Drinkwater |
Meneja wa Chelsea Antonio Conte anapanga kutumia pauni milioni 200
kuwasajili Danny Drinkwater, 27, kutoka Leicester, kiungo wa Arsenal,
Alex Oxlade-Chamberlain, 24, na mabeki watatu wa Southampton, Virgil Van
Dijk, 26, Cedric Soares, 25, na Ryan Bertrand, 28. (Express)
Chelsea
wamemuulizia beki wa kati wa Tottenham Toby Alderweireld, 28, ambaye
mazungumzo yake na Spurs kuhusu mkataba mpya yanasuasua. (Sunday Times)
Baada ya kumkosa Danny Drinkwater, meneja wa Chelsea sasa atamgeukia Grzegorz Krychowiak wa PSG. (Sun)
Atletico Madrid wapo tayari kutoa pauni milioni 50 kumsajili Diego Costa kutoka Chelsea. (Daily Mail)
Manchester City wapo tayari kuilipa Arsenal pauni milioni 70 ili kumsajili Alexis Sanchez, 28. (Mirror)
Manchester City watampa Alexis Sanchez, mshahara wa pauni 400,000 na kumfanya mchezaji anayelipwa zaidi England. (Sun on Sunday)
Barcelona
watalipa pauni milioni 36.5 za kutengua kipengele cha uhamisho cha Jean
Michel Seri, 26, na huenda wakakamilisha usajili wake ifikapo Jumatatu
kutoka Nice. (Mundo Deportivo)
Barcelona wamewaambia Liverpool
wana hadi siku ya Jumapili kukubali au kukataa dau la pauni milioni 118
la kutaka kumsajili Philippe Coutinho, 25, vinginevyo dau hilo
litaondolewa mezani. (Times)
Barcelona wameweka usajili wa
Philippe Coutinho kuwa kipaumbele na wanafanya kila jitihada kumpata
mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil. (Sport)
![]() |
Philippe Coutinho |
Barcelona watapanda dau jipya la pauni milioni 130, ingawa Liverpool
wanasema thamani ya Philippe Coutinho ni pauni milioni 140. (Express)
Luis Suarez amewaambia Barcelona kuwa kumsajili Philippe Coutinho "sio dawa" ya matatizo waliyonayo sasa hivi. (Liverpool Echo)
Paris Saint-Germain hatimaye wamefikia makubaliano na Monaco ya kumsajili Kylian Mbappe, 18, kwa pauni milioni 182. (Mundo)
Newcastle wanafikiria kupanda dau kumtaka mshambuliaji wa West Ham Andy Carroll, 28. (Mirror)
Manchester United, Arsenal na Liverpool zinamtaka Julian Draxler, 23, wa PSG. (Mirror)
Mkurugenzi
wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc amesema mshambuliaji
Ousmane Dembele atauzwa kwa bei inayofaa. (FourFourTwo)
![]() |
Ousmane Dembele |
Barcelona watalazimika kutoa pauni milioni 137 pamoja na marupurupu juu ikiwa wanataka kumsajili Ousmane Dembele, 20. (RAC 1)
Arsenal wamewapa AC Milan nafasi ya kumsajili kiungo Jack Wilshere. (Corriere dello Sport)
Real Madrid wamekataa dau la pauni milioni 68.5 kutoka kwa Juventus kutaka kumsajili Mateo Kovacic, 23. (AS)
Arsenal, Tottenham na Manchester City wanataka kumsajili kiungo wa Fenerbahce Oguz Kagan, 18. (Sun)
0 comments:
Post a Comment